Psalms 96:10-13


10 aKatikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.”
Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa;
atawahukumu watu kwa uadilifu.
11 bMbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;
bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
12 cmashamba na yashangilie,
pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.
Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;
13 ditaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja,
anakuja kuihukumu dunia.
Ataihukumu dunia kwa haki,
na mataifa katika kweli yake.
Copyright information for SwhNEN